Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amesema kwasasa anajifananisha na pombe aina ya ‘wine’ inavyokaa sana ndiyo inazidi kuwa kali kutokana na uwezo wake anaouonesha kipindi hiki.

Ibrahimovich amesema kuwa anatarajia kucheza mpira mpaka atakapofikisha umri wa miaka 50 ndiyo atastaafu kabisa kucheza lakini kwasasa bado kwani anaamini kiwango chake kipo juu.

Mshambuliaji huyo ameyasema hayo baada ya kumalizika kwa mechi ya ligi dhidi ya West Brom ambapo United ilishinda 2-0 na magoli yote yakifungwa na Ibrahimovic na kupelekea kufikisha jumla ya magoli 11.

Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 alijiunga na Manchester United akitokea klabu ya Paris Saint-German akiwa kama mchezaji huru na kufakikiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na mashetani hao wa Old Trafford.

Mshambuliaji huyo kwasasa amekuwa msaada mkubwa kwa Manchester United kutokana na upachikaji magoli ndani ya timu hiyo ambayo kwasasa inaonekana kukaa vizuri baada ya kushinda mechi tatu mfululizo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *