Shirikisho la kimataifa la riadha, IAAF, limepiga marufuku wanaraidha kubadilisha uraia wao kufuatia pendekezo lililotolewa na rais wa shirikisho hilo, Lord Coe.

Pendekezo hilo limedai kuwa mchezo huo umekuwa kwenye ‘hali mbaya’ kufuatia vitendo vya wachezaji wengi kubadilisha uraia wa nchi zao za asili na kuhamia kwenye mataifa yasiyo na wakimbiaji.

‘Sasa ni wazi kabisa kwamba sheria mbalimbali za uhamisho wa wakimbiaji hususani kutoka Afrika, kwamba sheria za sasa haziruhusu tena utaratibu huo’ amenukuliwa Coe.

Wakimbiaji kutoka nchini Kenya na Ethiopia ndio wanaotarajiwa kuathiriwa zaidi kwa sheria hiyo mpya.

IAAF imedai kuwa inaendelea kupitia sheria za sasa kuhakikisha zinatoa ulinzi wa kutosha kwa wanariadha. Zuio hilo la wanariadha kubadili uraia limeanza kufanya kazi mara moja na huenda likaanza kuathiri maombi yaliyokuwa yafanywe mwishoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo sheria hiyo haitoathiri maombi ya kubadili uraia ambayo tayari yanashughulikiwa na IAAF.

Zaidi ya wanariadha 20 wa Kenya wamekuwa wakiwakilisha mataifa mengine kwenye mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika jijini Rio de Janeiro mwaka jana.

Majina ya wanariadha wenye asili ya Kenya wanaowakilisha mataifa mengine:

Bahrain

Ruth Chebet, mshindi wa medali ya dhahabu jijini Rio kwa mbio za mita 3000 akivunja rekodi ya dunia.

Wengine walioiwakilisha Bahrain ni:

  • Abraham Rotich (800m)
  • Benson Seuri (1,500m)
  • John Koech (3,000m steeplechase)
  • Albert Rop (5,000m)
  • Rose Chelim (marathon)
  • Eunice Kirwa (marathon)
  • Eunice Chumba (marathon)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *