Mbunge wa Mikumi ambaye ni msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Professor Jay’ Jumatatu hii alitembelea ofisi ya WCB na kujionea uwekezaji uliyofanywa na rais wa label hiyo Diamond Platnumz.

Professor Jay akiwa na rais wa WCB, Diamond Platnumz

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Professor Jay amesema Diamond ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wa Tanzania.

“Diamond kama brand sasa hivi ana ofisi ambayo mtu akija amkutani baa kama zamani sisi Rose Garden, sasa hivi huwezi kumtaka kiofisi Diamond mkakutana baa au mnakutana Slipway mnasaini mkataba,” alisema Professor.

Aliongeza, “Hata client ukiongea naye anaona kabisa huyu msanii kweli yupo serious, kweli anajielewa kwenye level yake, kwa hiyo inaongeza sana thamani ya mtu, ni kitu ambacho wasanii wengi tunahitaji,”

Katika hatua nyingine, rapper huyo alimsifia Diamond kwa uamuzi wa kuwasaini wasanii wenzake na kuwasaidia.

“Lakini pia nimefurahia zaidi na nilimwambia, Diamond ni msanii mkubwa na anaipeperusha bendera ya Taifa kimataifa, ameamua kuwasaini wasanii wengine, yaani hataki kwenda peke yake, watu wanasema ukitaka kufanikiwa tembea peke yako ila ikitaka kufanikiwa zaidi ungana na wenzako wengi, yaani unaweza kwenda mbali zaidi. Kwa hiyo mtu kama Diamond kitendo cha kuwasaini wasanii kama Rich Mavoko, Raymond, akina Harmonize kwanza mwenyewe inampa changamoto kwa sababu ni watu ambao wanafandana nao kwa aina ya muziki ambao anafanya, na pia ana nia ya dhati na muziki wa Tanzania kwa kuwasaidia vijana wenzake” alisema Professor Jay.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *