Staa wa Bongo Fleva na mmoja wa wamiliki wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni DON miongoni mwa wasanii wa nchi hii.

Platnumz kupitia akaunti yake ya Instagram ameonyesha vito vipya vya thamani vyenye mchanganyiko wa almasi na dhahabu na kudai zina thamani ya zaidi ya $77,000 (TZS172m).

Mwaka jana staa huyo alitajwa kuwa na utajiri unaofikia fedha za kitanzania Bilioni 8 ingawa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja wa kuonyesha utajiri huo.

Hata hivyo Diamond Platnumz anatajwa kuwa mwanamuziki wa Tanzania mwenye mafanikio makubwa zaidi kifedha huku akiwa na mikataba mingi ya kimataifa kwaajili ya mauzo ya kazi zake binafsi na kazi za wasanii waliopo chini ya lebo yake ya WCB.

diamond-platnumz-1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *