Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu ameagiza Hotuba ya Kambi ya Upinzani kuhusu Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ihaririwe na kufuta maneno yote katika kurasa 17.

Zungu ametoa uamuzi huo leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu, hata kabla ya bajeti yenyewe kuwakilishwa na Waziri Dk Harrison Mwakyembe.

Zungu amesema amezipihitia hotuba zote na kubaini kuwa ile ya upinzani itakayowalishwa na Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ina masuala yaliyopo mahakamani ambayo yamekwishazuliwa katika bajeti zilizotangulia.

Amesema maneno yenye mwelekeo huo yakisomwa atachukua hatua kutokana na maneno mambo mengi kuwa mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *