Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameziagiza hospitali zote za mikoa kuhakikisha zinatoa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya kwa kutumia methadone ndani ya miezi sita.

Kauli hiyo ametoa alipotembelea kituo cha kuwahudumia watu wanaotibiwa kuacha dawa za kulevya kwa kutumia methadone kilichopo Hospitali ya Mwananyamala.

Pia Naibu waziri huyo amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuhakikisha kuwa kuna Daktari Bingwa wa Afya ya Akili kwenye kila mkoa ili kuanzisha na kusimamia vituo hivyo.

Dkt. Kigwangalla amesema kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaohitaji huduma hiyo kwa siku za hivi karibuni kutokana na kuongezeka kwa udhibiti wa dawa za kulevya, huku kukiwapo kwa taarifa kwamba wauzaji wa dawa za kulevya wameathiriwa kwa kupoteza mapato ya shilingi bilioni 70.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Kigwangalla amekemea baadhi ya viongozi wanaopotosha jamii kuhusu dawa hizo methadone.

Kwa upande wake muangalizi wa kituo hicho Dkt. Kasian Ndindindi amesema uwepo wa kituo hicho cha Mwananyamala kwa sasa umesaidia kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya 3,351.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *