Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amemshtumu Rais mteule wa Marekani Donald Trump kwa kitendo cheke cha kukosoa sera ya Ujerumani kuhusu wahamiaji barani Ulaya.

Hollande amesema kauli hiyo ya Trump si ya busara kwa sababu bara la Ulaya haliwezi kuingiliwa na Marekani kwenye maamuzi yake.

Rais huyo mteule wa Marekani katika mahojiano yake amesema kuwa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel alifanya kosa kubwa kwa kuwaruhusu wahamiaji kuingia nchini mwake kwa wingi.

 Kwa upande wake Merkel amesema kuwa bara la Ulaya linatakiw kuachwa lijifanyie maamuzi yake wenyewe na siyo kuingiliwa kama anavyotaka kufanya Trump.

Naye Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alishutumu tamko hilo la Trump huku akisema kuwa Trump akustahili kuwa rais wa Marekani.

Vile vile Trump amezua wasiwasi miongoni mwa viongozi wa nchi wanachama wa muungano wa kujihami wa mataifa ya Magharibi (Nato) kwa kusema kwamba muungano huo umepitwa na wakati.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *