Hillary Clinton amekubali rasmi kuwa mgombezi wa Urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, huku akisema wakati wa kupambana na mpinzani wake sasa umeanza rasmi.

Alitoa wito kwa wanachama wote wa Democratic kuungana naye huku akimkebehi mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump.

Katika madai yake kuwa ni yeye pekee anayeweza kuyasuluhisha matatizo ya Marekani na amewataka waamarekani wote kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua mataizo yote.

Awali, bintiye Chelsea Clinton alikuwa ametoa hotuba na kumsifu sana mamake huku akisema ni mwanamke ambaye huwa hasahau anawapigania akina nani.

“Watu huniuliza kila wakati, huwa anawezaje kufanya haya ni kwa sababu huwa hawasahau watu anaowatetea,” amesema mtoto huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *