Mwanamke mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mchumba kwa muda mrefu.

May Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan amesema kuwa anaugua ugonjwa huo lakini hajakubali sababu hiyo kuhujumu ndoto yake ya kuolewa.

Amesema kwamba wakati unapohisi kwamba huna miaka mingi ya kuishi huna budi kujifanyia maswala ambayo yamekuwa ndoto yako.

Pia amesema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa.

Ameongeza kwa kusema kuwa anasema kuwa wapiga picha walimshauri kupiga picha katika studio lakini yeye akawaambia kwamba anataka picha sawa na zile za harusi.

Kwa sababu yeye huugua saratani ya matiti hulazimika kwenda hospitali mara tatu kwa wiki ili kudungwa sindano mbali na kutibiwa kwa kutumia kemikali.

Anaongezea kwamba kwa muda mrefu hakuweza kusimama kwa miguu miwili na kuvaa suruali ndefu.

Amesema kuwa hakuweza kutembea na kwamba nywele alizo nazo sio nywele zake asilia.

Amemaliza kwa kusema kwamba anatumia habari yake kuwapa moyo wanaougua kwamba maisha sio mabaya sana kwasababu watu wengi wanaougua huwa na wasiwasi wataishi kwa muda gani na lini watafariki ama iwapo matibabu wanayopata yanafanya kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *