Kiungo wa Ubelgiji na klabu ya Chelsea, Eden Hazard ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba katika ligi kuu nchini Uingereza.

Tuzo ya kocha bora mwezi Oktoba ikienda kwa kocha wa Chelsea, Antoine Conte ambaye ameshinda tuzo ya kocha bora wa EPL.

Chelsea imeshinda mechi zote 4 za ligi kuu katika mwezi huo, wakifunga magoli 11 na hawakuruhusu kufungwa goli hata moja, huku mchezaji Hazard akiwa amecheza mechi 4,akifunga goli 3 na kutoa Assist 1.

Siku ya jumamosi Chelsea itacheza dhidi ya Middlesbrough kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza katika uwanja wa Riverside Stadium.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *