Kundi maarufu linaloipinga serikali ya Cuba limesitisha maandamano yake ya kila wiki kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi na tatu kufuatia kifo cha Fidel Castro ambaye wao wamekuwa wakimpinga kwa miaka yote.

Kiongozi wa kundi hilo la wanawake maarufu kama Ladies in White, Berta Soler, amesema ametaka kutoa fursa kwa wengine kuomboleza na hivyo hatasheherekea kifo cha mtu yeyote.

Maandamano hayo ya wanawake ya kila wiki ni kwa lengo la kuwaunga mkono waume zao waliofungwa kwa sababu ya kuipinga serikali.

Kumekuwa na hali ya simanzi katika mji mkuu wa Havana siku kilipotangazwa kifo cha Fidel Castro.

Baadhi ya raia mjini Havana wamesema wameanza kukubaliana na hali halisi huku wakianza siku tisa za maombelezo kufuatia kifo cha rais huyo wa zamani wa Cuba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *