Rais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe Spunda amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi juu ya utata wa jina lake unaozidi kuvuma mitandaoni.

Utata huo unadaiwa kutokana na mkuu huyo wa mkoa kutumia cheti cha mtu mwingine cha kidato cha nne kujiendeleza kielimu.

Rungwe amemtaka Makonda kuweka ukweli mezani na kuacha kupiga chenga za mchangani kwa maana akiendelea kukaa kimya watu wanazidi kuamini uvumi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Kwa upande mwingine, Rungwe ambaye ni wakili ametoa ushauri wa kisheria kwa watu wenye ushahidi na suala hilo kwenda mahakamani kwa kuwa sheria inaruhusu mashtaka binafsi, ingawa bado Jamhuri itahitajika zaidi kuisimamia kesi hiyo.

Pia Kwa upande mwingine Mzee Spunda amemuomba Rais Magufuli kuliingilia kati suala hilo kama alivyofanya kwa maafisa wengine wa serikali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *