Mchezaji wa zamani wa Timu ya OKC Thunder ya ligi kuu ya Marekani (NBA) Mtanzania Hasheem Thabeet kwa sasa amejiunga na Timu ya Yokohama B Corsairs ya Ligi kuu ya kikapu ya Japan.

Hasheem ambaye kwa mara ya mwisho alikuwa akicheza katika katika Ligi D ndani ya klabu ya Grand Rapids Drive ya nchini Marekani amesajiliwa kwa dau ambalo mpaka sasa halijawekwa wazi na tayari amekabidhiwa Jezi yenye namba 34 katika timu hiyo.

Mchezaji huyo alitamba na kulitangaza taifa katika mchezo wa kikapu baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu ya NBA nchini Marekani katika msimu wa 2009 akiwa na timu ya Memphis Grizzlies.

Alifanya vizuri pia akiwa na timu ya Oklahoma City Thunder katika msimu wa 2012 hadi 2014, lakini baada ya hapo alionekana kushuka kiwango chake na kutupwa katika ligi ya kujiendeleza kwa ajili ya kupandisha kiwango ili aweze kurudi Ligi ya NBA.

Hasheem Thabit Alizaliwa tarehe 16 mwezi Februari mwaka1987

Ligi ya kikapu ya Japan B-League inatarajiwa kuanza kesho ijumaa wiki hii, na Hasheem yupo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili huo ili kukipiga rasmi katika timu ya Yokohama B Corsairs ya Japani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *