Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmorapa jana ameonekana akimganda mmiliki wa kampuni ya kinywaji cha Swala.

Tukio hiyo la Harmorapa kumganda mmiliki huyo ilikuwa katika viwanja vya Escape One Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamejiri baada ya kusambaa kwa taarifa za kupewa dili nono na kampuni inayozalisha kinywaji cha Swala.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Hamorapa, imeweka Ujumbe akijinadi kwa mashabiki wake kuwa yupo na mzungu wake bosi wa kijanywaji hicho.

Kutokana na tabia za mwanamuziki huyo kupeenda kiki, mashabiki wanamshauri Hamorapa kufanya kazi nzuri za sanaa na kuachana na kiki zisizo na kichwa wala miguu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *