Mwanamuziki chipukizi wa Bongo Fleva, Harmorapa amesema kuwa amenunuliwa nyumba kali ya kuishi maeneo ya mikocheni Jijini Dar es Salaam na uongozi wake unaomsimamia kazi zake.

Harmorapa amesema mpaka sasa hajafahamu kiasi kilichogharimu kutumiwa katika kununuliwa nyumba hiyo kwa kuwa yeye amepewa kama zawadi.  

Mwanamuziki huyo amesema kuwaYaah nimenunuliwa nyumba maeneno ya Mikocheni na boss wangu Irene Sabuka, nyumba ipo fresh inavyumba viwili na sitting room na bafu na kila kitu ambacho staa anastahili kumiliki na menejineti imeamua kufanya hivi ili niweze kuwa kwenye nyumba ya hadhi ya staa kama mimi”. 

Kwa upande mwingine msanii huyo amebainisha kuwa alianza kuchana tangu kitambo lakini muda wa kutoka ndiyo ulikuwa bado haujafikia kwake hivyo amewataka watu wampe -support kwakuwa yeye pia ni msanii kama wasanii wengine hapa Tanzania.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Kiboko ya Mabishoo’ aliomshirikisha Juma Nature.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *