Mwanamuziki chipukizi wa Bongo Fleva, Harmorapa amesema kuwa hana mpango wa kubadilisha jina lake lililomtambulisha.

Hamorapa amesema maneno ya watu kuwa ameamua kujiweka upande wa Alikiba ingawa ameshindwa kujizuia kuonesha mahaba yake kwa msanii huyo.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Mi sijali watu watakaosema mimi ni team Kiba kwa kuwa niliamua kumpigia Alikiba magoti ile ilitokana na heshima na amefanya vitu vikubwa na kuwakilisha nchi yetu vizuri, kwa mimi namuhusudu saana Ali Kiba’

Hata hivyo Hamorapa amewapa ujumbe watu ambao wamamsema vibaya kwamba hawezi kuimba, wanapaswa kutambua kwamba wanavyomsema vibaya wanamfanya aongeze juhudi na kujua vingi kila siku kwa kutumia zile ‘diss’ wanazompa.

Harmorapa kwasasa anatamba na wimbo wake mpya ‘Kiboko ya Mabishoo’ aliomshirikisha mkongwe Juma Nature.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *