Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmorapa amefunguka na kusema kuwa ukimya wake kwenye muziki unasababishwa na ubusy wa biashara zake.

Harmorapa amesema hayo baada ya watu kuhoji ukimya wa mwanamuziki huyo asiyeishiwa na vituko kwenye tasnia ya muziki wa Bongo.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa ukiachana na maisha ya muziki , kuna kitu kingine anafanya tofauti na icho hivyo kwa muda huu mambo ya biashara yamemfanya kuwa busy ila anakaribia kurudi hivi karibuni na mashabiki wakae mkao wa kula.

Pia amesema kuwa watu wanabidi wajue kuwa kuna maisha nje ya muziki,”watu waelewe  kuwa sipo kimya kuwa nimefulia, sasa hivi niko busy na biashara na pia nina safiri sana,ile kuonana tu ni bahati.Project zangu zinaendelea kama kawaida, na wiki ijayo naachia dude jipya, watu wajue mimi nipo ,tatizo wamezoea kuwa harmorapa kafanya hivi mara kafanya vile, kwa sasa niko busy na biashara na muziki wangu bado upo sana.kama kutrend kila siku na-trend, kila siku naingia instagram,nakuta tu mtu amenipost kwaiyo nakuwa najua kumbe bado nipo machoni pa watu.Bado mimi nipo  na muziki upo na vitu vitaendelea”.

Kwa muda sasa Harmorapa amekuwa kuwa kimya , tofauti na jinsi alivyokuwa akichukua vichwa vya habari katika vyombo vya habari , na kuna baadhi ya watu wakaanza kusema kuwa inawezekana atakuwa amefulia, hivyo harmorapa kaamua kuwajibu wanaomzushia habari hizo na kwamba hivi karibuni anatoa wimbo mpya hivi wasubiri kitu kipya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *