Mwanamuziki wa hip hop bongo, Harmorapa amefunguka kwa kusema kuwa kwasasa hayupo katika maelewano mazuri na mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, P Funk.

Harmorapa amesema kuwa kwasasa hawana mawasiliano mazuri na P Funk, kwani kuna mambo ambayo yalitokea, yaliyosababisha kutoelewana kwao,

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Nikimzungumzia Majani, kwenye maisha mtu unapitia sehemu nyingi, mfano mimi nafanya kazi kwa mtu halafu maslahi siyaoni, nafanya kazi kwa jasho najituma halafu yeye ndiyo ananufaika, halafu anakuona wewe humfai, na mwisho wa siku ndiyo inakuwa hivyo”.

Harmorapa kwa sasa ameachia wimbo wake ambao umeonekana kumchana P Funk Majani ambaye alimsimamia kwenye kazi yake ya Nundu, na kumuunganisha na baadhi ya watu ili aweze kufanikisha kazi zake za muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *