Staa wa Bongo Fleva, Harmonize amesema kitendo cha Dully Sykes kumpigia simu na kumwambia anataka kumshirikisha katika kazi yake kilimfanya aone fahari sana.

Staa huyo amesema kipindi anapigiwa simu na Dully Sykes alikuwa nje ya nchi akifanya ‘shooting’ akaahidi akirudi lazima ashiriki kazi hiyo.

Harmonize amesema alikuwa Johanesburg akapigiwa simu na Dully Sykes kwamba anataka afanye kazi na yeye alifarijika kwa kuwa msanii huyo ni moja kati ya watu ambao wamefanya vizuri sana katika tania ya muziki wa Bongo Flava.

Staa huyo kwasasa anatamba na wimbo wake “Matatizo” amesema alijiuliza sana kwasababu kuna vijana wengi wanafanya vizuri katika muziki kwasasa lakini Dully Skykes akaamua kumfuata yeye.

Kwa upande mwingine Harmonize amesema kwamba mashabiki wanaomfananisha na Diamond Platnumz wanakosea kwa sababu yeye hafananii chochote na mkali huyo wa WCB zaidi ya kuwa naye karibu kikazi.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *