Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize kutoka lebo ya WCB amesema kuwa katika harakati zake za kutafuta maisha alishawahi kuwa dereva wa bodaboda kabla ajafanikiwa kwenye muziki.

Harmonize amesema aliifanya kazi hiyo katika kuhakikisha anaendesha maisha yake kabla ya kutoka kwenye muziki anaofanya kwasasa.

Mkali huyo wa ‘Bado’ amesema kuwa anakumbuka mwaka 2011 alikuwa akifanya kazi hiyo ya kuendesha pikipiki na kubeba abiria ndiyo maana ana uzoefu mzuri wa kuendesha Pikipiki kutokana na kazi yake hiyo aliyoifanya kwa kipindi cha nyuma.

Harmonize amesema “Unajua mimi nilishawahi kuwa dereva bodaboda nakumbuka ilikuwa mwaka 2011 nilikuwa nafanya kazi ya kubeba watu na Pikipiki hivyo nina uzoefu mzuri tu wa kuendesha Pikipiki, nilikuwa nabeba abiria hapa na pale najipatia riziki ndiyo maana hata katika video yangu ya ‘Bado’ niliona niendesha tu ile pikipiki kwa kuwa nilikuwa na uzoefu wa kuendesha pikipiki,’.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Matatizo’ aliyoelezea maisha yake ya nyuma kabla ajawa staa wa muziki hapa Bongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *