Staa wa Bongo fleva, Harmonize amefunguka kwa kusema Master J alimuambia hajui kuimba baada ya kujitokeza kwenye shindano la BSS mwaka 2012 na kutoendelea tena kwenye shindano hilo.

Harmonize amesema kuwa baada ya kuambiwa hajui kuimba katika shindalo hilo alijiangalia na akajikuta ni kweli alikuwa hajui kuimba wakati huo lakini hakukata tamaa kwenye suala la uimbaji.

 Muimbaji huyo alishiriki shindano la BSS mwaka 2012 na Walter Chilambo kuibuka na ushindi na kuondoka na taji hilo.

Harmonize amesema hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutokubaliana na matokeo kutokana na  alivyokuwa anaimba kwenye BSS, huku akiongeza kwamba hata angekuwa mtu mwingine angemuambia hajui kuimba kipindi hicho lakini akazidi kufanya mazoezi.

Master Jay
Master Jay

Muimbaji huyo amesema kauli ya Master J haikumkatisha tamaa kwani aliendelea kupambana na kutafuta njia yakutokea kwenye muziki.

Pia alisema alikuwa anahudhiria show mbalimbali ili kujifunza jinsi ya kuperfom katika matamasha mbalimbali.

Hamronize kwasasa anatamba na nyimbo yake inayokwenda kwa jina la ” Matatizo” ambapo inaendelea kufanya vizuri kwenye vituo mbali mbali vya radio na TV hapa nchini pamoja na baadhi ya nje za nchi.

Kwasasa mwanamuziki huyo yupo chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na nguli wa muziki nchini Diamond Platnum ambapo amekuwa mwanamuziki wa kwanza kusainiwa na lebo hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *