Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameamua kutoa ya moyoni kuhusu wasanii wa muziki wa Bongo Fleva kutokuwa na ushirikiano hasa kupeana sapoti ili kukuza muziki wa Bongo Fleva kimataifa.

Harmonize ameeleza kuwa moja ya kitu kinachopelekea muziki wetu kutokuwa mkubwa ni chuki zisizo na maana miongoni mwa wasnaii.

Ametolea mfano wa wasnaii wa Nigeria akiwataja Wizkid, Burna boy na wengine akisema huenda wako busy ndio mana hawagombani.

Wasanii wa Bongo Fleva wanapishana humu humu ndio mana wanarushiana maneno.

Pia Harmonize amefunguka kuwa wimbo wake wa Single Again unaenda kufungua Milango yake ya kimataifa.

Mbali na hivyo Staa huyo amedai kuwa hata wimbo huo usingekuwa na mapokezi makubwa asingeumia kwani anachukulia kama nafasi ya kufikia ndoto zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *