Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kusema kuwa mpenzi wake Sarah ana ujauzito mkubwa na muda wowote anaweza kujifungua.

Harmonize amesema hayo wakati akipafomu kwenye Jukwaa la Jipoze Concert lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Pia Harmonize ametoa sababu ya kuachana na Jacquline Wolper baada ya kumfumania na meseji tofauti tofauti za wapenzi wake akiwemo mmoja aliyekuwa China na mwingine Burundi pamoja na kuomba penzi la Diamond Platnumz.

Harmonzie amesema alipanga asimwambie lakini anasema vingi, amekuwa akifanya mahojiano na kumsema vibaya mpenzi wake.

Harmonize amesema kuwa kitendo cha Wolper kumwita mpenzi wake Sara kama Sponsor kina muumiza sana kwani yeye ni mtu ambaye anampenda na anatarajia kupata mtoto baada ya kushika ujauzito.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *