Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amepata maneno ya ushauri kutoka kwa mashabiki wake wakimtaka kukaza buti na asibweteke baada ya kushinda tuzo ya AFRIMMA.

Wiki iliyopita mwanamuziki huyo ameshinda tuzo ya Afrimma (African Muzik Magazine Awards), zilizofanyikia Dallas nchini Marekani katika kipengele cha Msanii Bora Chipukizi kutoka Afrika Mashariki.

Mashabiki hao wamemtaka kukaza buti huku wakimmwambia kuwa akilegea kidogo tu msanii mwenzake kutoka kwenye lebo yao ya WCB, Ray Vanny atamfunika.

Mashabiki hao walimpa ushauri huo kupitia kwenye mitandao ya kijamii lakini pia walimpongeza kwa ushindi huo na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Wengine walioshinda tuzo hizo kutoka Tanzania ni pamoja na Diamond Platnumz aliyechukua Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki na DJ D- Ommy aliyechukua Tuzo ya DJ Bora wa Afrika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *