Mwanamuziki nyota kutoka WCB, Harmonize amekiri kwa mara ya kwanza kuachana na mpenzi wake muigizaji, Jacqueline Wolper.

Kauli hiyo ya Harmonize imekuja kufuatia kusambaa habari za kuachana kwake na muigizaji huyo wa Bongo Movie.

Harmonize amsema ni kweli wameachana japo alikuwa na malengo naye na asingependa kulizungumzia sana hilo kwa undani zaidi.

Amesema kuwa ”Siko kwenye mahusiano kwa sasa ni kweli nimeachana na Wolper’na kusema ukweli nilikuwa na mipango mingi na Wolper nyumbani nikampeleka lakini kila mwanadamu ana nyongo kwasasa sipo naye tena

Jacqueline Wolper-
Jacqueline Wolper-

Mwanamuziki huyo amesema kwasasa hayupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamke yeyote kwani amejikita kwenye kazi zake za kimuziki.

Kuna taarifa zilisambaa kuwa Harmonize ana mahusiano ya kimapenzi na mwanamke wa kizungu ambaye amempa ujauzito ikiwa ndiyo sababu ya kuachana na Wolper lakini mwanamuziki huyo amekana kuwepo kwa suala hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *