Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amedai kuwa hajawahi kusikia habari zozote kuhusu bosi wake Diamond kutoka kimapenzi na Jacqueline Wolper.

Harmonize amesema kuwa ajawahi kusikia kama mpenzi wake huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Diamond Platnumz.

Mwanamuziki huyo amesema hayo baada ya habari kuenea kuwa Diamond alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Jacqueline Wolper kabla ajaanza mahusiano na Harmonize ambaye ni mwanamuziki wa Diamond.

harmonize

Harmonize amesema kuwa wakati anataka kuanza mahusiano ya kimapenzi na Jacqueline Wolper alimuuliza Diamond kuhusu Muigizaji huyo na Diamond akamwambia hakuna tatizo lakini hakumwambia kama alishawahi kudate nae.

Mwanamuziki huyo na Jacqueline Wolper wapo katika mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu licha kuibuka kwa habari za kuachana kwa wawili hao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *