Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefuta Tattoo ya Picha ya aliekuwa Mpenzi wake Kajala Masanja na mtoto wake Kajala aliokuwa amechora kwenye Mguu wake wa kulia.

Kupitia video alioishare katika ukurasa wake wa Instagram akiimba Wimbo wake mpya wa Single Again ukitazama vizuri katika Mguu aliokuwa amezichora Sura hizo kuna Tattoo nyingine ameichora juu yake.

Mwanamuziki huyo ameamua kufuta tattoo hizo kutokana na kutokuwa na mahusiano ya wawili hao ambao kwasasa awapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Harmonize aliwahi kuchora tattoo ya Kajala kwa kuandika kifupi cha neno ya Kajala ‘K’ lakini baada ya kuachana aliifuta tattoo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *