Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amesimulia namna ilivyobaki kidogo sana kumuoa mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wake.

Harmonize ameendelea kwa kusema kuwa chochote atakachosema mzazi (Mama au Baba) wasikilize sana hata kama sio wazazi wako.

Ameendelea kuwa Wazazi wanaona mbali sana hasa kama kuna kitu unafanya. Mzazi anaona kabisa hapa unaenda kufanikiwa au huwezi kufanikiwa.

Na ukiona mzazi amekukataza kufanya kitu fulani usifanye kwa sababu ameona mbeleni kukoje.

Mwanamuziki huyo alikuwa kwenye uhusiano na muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja ambaye kwasasa wameachana na hawapo kwenye uhusiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *