Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesafiri kwenda Singapore kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Kiongozi huyo alihutubia wajumbe katika mkutano mkuu wa Baraza la uchumi Duniani Afrika Kusini wiki iliyopita.

Mugabe anatarajiwa kurejea nyumbani kwa wakati kuweza kuhudhuria mazishi ya jaji mkuu wa zamani Godfrey Chidyausiku.

Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa atatekeleza majukumu ya rais Mugabe atakapokuwa nje ya nchi hiyo.

Licha ya umri wake, chama tawala cha Zanu-PF kilimuidhinisha Mugabe kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Katika mkutano Februari, mkewe, Grace Mugabe alisema kuwa Siku moja Mungu atakapoamua kwamba Mugabe afe basi tutakuwa na maiti yake kama mgombea kwenye karatasi ya kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *