Mhubiri aliyefahamika kwa jina la Pasta Patrick Mugadza raia wa Zimbabwe amekamatwa na maafisa wa polisi baada ya kutabili kuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugame atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.

Wakili wa Mhubiri huyo Gift Mtisi amesema kuwa Pasta huyo amekamatwa akiwa mahakamani mjini Harare siku ya jana ambapo alikuwa ameenda kwa kesi nyingine dhidi yake.

Pasta Mugadza aliandaa kikao na wanahabari wiki iliyopita ambapo alitabiri kwamba Rais Mugabe atafariki mwezi Oktoba 17 mwaka huu.

Kumfanyia mzaha Rais Mugabe au kutoa unabii au ubashiri kumhusu ni jambo hatari nchini Zimbabwe.

Mwaka 2015, Mugadza alikamatwa na kuzuiliwa kwa karibu mwezi mmoja baada ya kujitokeza hadharani na bango lililokuiwa na ujumbe uliomwambia Mugabe kwamba watu wamekuwa wakiteseka chini ya utawala wake.

Siku ya maadhimisho ya uhuru mwaka jana, alitoa mahubiri akiwa amejifungia kwenye boriti ya taa nje ya duka kubwa zaidi la kibiashara mjini Harare akisema hiyo ilikuwa ishara ya raia kukandamizwa Zimbabwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *