Mwanamuziki nyota wa Mareakani, Jason Derulo leo septemba 21 anasheherekea siku yake ya kuzaliwa baada ya kufikisha miaka 27.

Mwanamuziki huyo pia ni mtunzi wa nyimbo na dansa ameanza kujikita kwenye suala zima la uimbaji kuanzia mwaka 2009 pbaada ya kusimama kama msanii anayejitegemea ambapo amefanikiwa kuuza platinum baadhi ya single zake.

Derulo alianza kutoa nyimbo yake ya kwanza mwaka 2009 ilijulikana kwa jina la ‘Watcha Say’ ambayo ilifanya vizuri mpaka kufikia mauzo ya platnum kutokana na nyimbo hiyo kugusa mashabiki wengi pamoja na kununuliwa sana.

Mwanamuziki huyo pia amewaandikia nyimbo baadhi ya wasanii wakubwa nchini Marekani kama vile Diddy, Danity Kane, Donnie Klang, Sean Kingston, Cassie, na Lil Wayne ambao nyimbo zao zilifanya vizuri masikioni mwa mashabiki.

Derulo aliwahi kuwa na mahusiano na mwanamuziki, Jordin Sparks ambapo uhusiano huo ulidumu kwa miaka mitatu na kuachana mwaka 2014.

Tovuti hii inamtakia heri ya siku ya kuzaliwa kwa mwanamziki huyo Mwenyezimungu amfanyie wepesi katika maisha yake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *