Mwanamuziki wa Bongo fleva, Dogo Janja ‘Janjaro’ leo Septemba 15 anasheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Mkali  huyo wa wimbo wa “Kidebe” alizaliwa tarehe kama ya leo jijini Arusha ambapo ni asili ya wazazi wake.

Dogo Janja yupo chini ya Tip Top Connections ambapo kwasasa anaonekana kufanya vizuri kwenye anga ya muziki wa Bongo fleva kutokana na vibao vyake kugonga nyoyo za mashabiki wake.

Mwanamuziki huyo alianza muziki toka akiwa mdogo baada ya kiongozi wa Tipo Top, Madee kugundua kipaji chake na kumuingiza kwenye kundi hilo lenye maskani yake maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam.

Dogo Janja: Akiwa na baba yake mzazi
Dogo Janja: Akiwa na baba yake mzazi

Dogo janja kwasasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya “Kidebe” ambao umekuwa habari ya mjini kutokana na mabadiliko aliyoonesha kwenye wimbo huo baada ya kuchanganya radha ya hip hop na kuimba.

Tovuti hii inamtakia Heri ya siku ya kuzaliwa Dogo Janja na Mungu amfanyie wepesi katika harakati zake za kimaisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *