Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametoa siku saba kwa wachimba kokoto wa eneo la Boko Chama kuondoa mawe yaliyopo kwenye eneo hilo ili kupisha ujenzi wa dampo la kisasa.

Hapi ametoa kauli hilo wakati alipotembelea eneo hilo na kukagua ambapo hapo awali wachimbaji hao walitakiwa kuondoka lakini hawakufanya hivyo.

hapi

Pia amewataka wachimbaji hao kuacha kuchimba kokoto eneo hilo kutokana na mvua zinazoendelea katika jiji la Dar es Salaam na uhenda kukasababisha mmomonyoko wa udongo kwenye machimbo hayo.

Amesema kuwa amewaagiza maafisa wa mazingira na mipango miji waunde timu ili waangalie uwezekano wa kutengeneza dampo eneo hilo ambapo kwasasa wakazi wa eneo hilo wanatumia dampo la Pugu Kinyamwezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *