Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope amefuta uamuzi wake wa kujiuzulu ndani ya klabu hiyo.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kuenea taarifa za kujiuzulu kwa Hanspope.

Kupitia akaunti yake ya Intagram Haji Manara amethibitisha kwa kusema kuwa Hanspope amerudi kundini.

Ujumbe huo ulisomeka kama ifuatavyo “Rasmi Hanspope arejea kundini, afuta uamuzi wake wa kujiuzulu na ndio maana ‘fans’ wetu nawaomba mtulie hakuna kitakachoharibika, ni upepo mbaya ulipita na sasa umetulia, karibu tena kamanda Pope.

Jana zilienea taarifa kuwa Hanspope amejiuzuru nafasi ndani ya klabu ya Simba lakini hajaweka bayana chanzo cha kujiuzuru kwake.

Hanspope alipoulizwa kuhusu suala la kujiuzulu kwake amesema kuwa wawaulize Simba yeye hana la kujibu.

Hanspope bado hajathibitisha kama kweli ametengua uamuzi wake wa kujiuzulu ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *