Kocha mkuu wa Yanga SC, Hans van Pluijm amesema kuwa sasa wanaelekeza nguvu zao katika michezo inayofuata ili kubadili matokeo yaliyo mazuri ukiwemo dhidi ya Simba mwishoni mwa wiki hii.

Pluijm amesema kama wanahitaji kucheza michuano ya kimataifa ni lazima wapate matokeo mazuri.

Kocha huyo ameendelea kusema anaiheshimu Simba lakini hana hofu nayo, kwani ni lazima timu hiyo ikae chini kwa kuwa wanajipanga kuchukua pointi tatu.

Kocha Pluijm amesema wanachotakiwa kufanya ni wachezaji kucheza kwa kujiamini na ukakamavu jambo ambalo amekuwa akilisisitiza kwa wachezaji wake mara kwa mara sio tu katika mchezo huo bali michezo yote.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuweka kambi Pemba kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ni muhimu kwa timu zote kwani Yanga itahitaji ushindi ili kurudi kwenye mstari katika mbio za kutetea taji lake huku Simba ikihitaji ushindi ili kujiweka sawa katika kuwania taji la kwanza baada ya miaka minne.

Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 10 huku Simba ikiongoza kwa pointi 16 na Stand United ikishika nafasi ya pili kwa pointi 12.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *