Aliyekuwa kocha wa Yanga, Hans Van der Pluijm amekubali kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo huku nafasi yake ikichukuliwa na George Lwandamina kutoka Zesco ya Zambia.

Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga amesema uongozi wa klabu hiyo ulikuwa kwenye mazungumzo na kocha Hans ili aridhie maamuzi hayo, na hatimaye amekubali kufanya kazi na kocha George Lwandamina.

Pia Sanga amesema hatma ya Mwambusi bado haijafahamika kwa kuwa nafasi ya kocha msaidizi itategemea matakwa ya kocha mkuu.

Sanga ameongoza kwa kusema kuwa uamuzi huo ni kwa ajili ya kuboresha kikosi hicho, na kwamba ni mabadiliko ya kawaida katika uendeshaji vilabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *