Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Vicent Mashinji amesema kuwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anaendelea vizuri na amezinduka na kujitambua.

Dk Mashinji amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akielezea tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu.

Mashinji amesema kuwa amezungumza na mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambaye yupo jijini Nairobi nchini Kenya ambaye aliongozana na Tundu Lissu kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kushambuliwa na risasi jana.

Katibu mkuu huyo amesema kuwa tukio hilo alikuwatisha bali linawafanya wasonge mbele katika masuala ya siasa.

Tundu Lissu alifyatuliwa risasi 32 lakini risasi zilizompata ni tano ambapo mbili zilimpata tumboni, mbili nyingine mguuni na moja mkononi.

Kwasasa Tundu Lissu yupo jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya matibabu zaidi katika hospitali ya Aga Khan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *