Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaendelea vizuri na ameweza kula na kuongea na watu tofauti.

Lema ametumia ukurasa wake wa Twitter kuelezea hali ya Mbunge huyo ambapo mara kwa mara amekuwa akitumia ukurasa huo kutoa taarifa za afya ya mbunge huyo.

Lema kupitia akaunti yake ameandika “Mh Lissu anaendelea vyema hospital . Leo ameweza kula vizuri na kuongea na watu wengi zaidi. Asanteni kwa sala zenu. Mungu awabariki sana,”

Tundu Lissu ambaye kwasasa jijini Nairobi nchini Kenya akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi eneo la ‘area D’ mjini Dodoma na watu wasiojulikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *