Nahodha wa Simba, Jonas Mkude anaendelea vizuri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako amefanyiwa vipimo na kupata matibabu kwa ujumla.

Mkude alikuwa kati ya watu sita waliopata ajali iliyotokea jana na shabiki mmoja wa Simba, Shose Fidelis amepoteza maisha.

Ajali hiyo ilitokea siku moja tu baada ya Mkude kuingoza Simba kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Kiungo huyo alifikishwa Muhimbili kwa matibabu zaidi ili kupata uhakika wa afya yake baada ya kupata ajali hiyo eneo la Dumila mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi mmoja wa Simba amesema kuwa hali yake inaonekana kuimarika na imeelezwa jana alikuwa akilalama sana maumivu lakini sasa ana nafuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *