Baada ya kupata ajali mkoani Shinyanga, mchekeshaji Emmanuel Mathias maarufu kama MC Pilipili hali yake inaendelea vizuri.

Kauli hiyo imetolewa na Daktari wa Hospitali ya Bugando, Dk. Cloud MC Pilipili yupo chini ya uangalizi na anaendelea vizuri na matibabu.

Awali hapo zilitoka habari kuwa mchekeshaji huyo yupo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu akisubiria kufanyiwa vipimo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alithibitisha kutokea ajali hiyo ambapo alieleza kuwa Mc Pilipili alikuwa akimkwepa mwendesha baiskeli katika Kijiji cha Bubiki, Kata ya Mondo mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *