Afisa Habari wa Simba SC, Haji Manara amefunguka na kudai sio kweli ana mpango wa kutaka kuikacha Klabu yake ya wekundu wa Msimbazi na kuitaka jamii kuzipuuza taarifa hizo pindi watakapokutana nazo au kusikia.

Manara amebainisha hayo mchana wa leo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kuwepo na taharuki kubwa kwa wapenzi wa soka kutokana na kusikia taarifa zinazomuhisha kiongozi huyo kutaka kuikimbia Simba bila ya kuwepo na sababu maalum juu ya jambo hilo.

“Siondoki Simba na naomba muelewe hivyo, ninafanya kazi sehemu sahihi na wakati sahihi. Rafiki zangu na washabiki wa klabu muelewe hivyo, walichokitangaza ni uzushi nawezaje kuwaacha simba kipindi hiki muhimu”,.

Jibu hilo la Manara limeweza kurudisha furaha na bashasha kwa wapenzi wa klabu ya Simba kwa kile wanachokiamini kuwa kiongozi huyo anawapa hamasa nyingi wakati wa kuelekea mchezo hata baada ya matokeo vile vile.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *