Mwanamuziki wa Bongo Fleva, H- Baba amefunguka na kusema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa Simba wameonesha nia ya kumuhitaji kwenye kikosi chao.

H- baba ambaye alikuwa nahodha wa timu ya soka ya Bongo Fleva ambayo ilipambana na timu ya Bongo Movie katika mchezo wa hisani uliochezwa mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, amesema neema hiyo ni kutokana na uwezo aliouonesha katika mchezo huo.

H Baba baada ya kuingoza vyema timu ya Bongo Fleva na kuibuka na ushindi wa bao 6 dhidi ya 5 alisema alipata nafasi ya kukutana na moja ya kiongozi wa Simba ambaye alionesha kukubali uwezo wake.

Kikosi cha Bongo Fleva
Kikosi cha Bongo Fleva

Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram H- Baba ameandika “Baada ya ushindi dhidi ya Bongo Movie nilikuwa na kiongozi wa Simba Kaburu tukiongea mawili matatu, kaniuliza ‘kwa mpira niliocheza leo na mabao mazuri niliyopachika juzi upo tayari kutua Simba dirisha dogo? “.

Mbali na hapo H Baba alizidi kuonesha kuwa huenda Wekundu wa Msimbazi wamevutiwa na uwezo wake kwani baadaye alikuja wauliza mashabiki wa Simba kama wataweza kumpokea katika klabu hiyo na kuwaahidi kutupia mabao kila mechi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *