Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Hamis Baba maarufu kama H Baba amemuandikia ujumbe wa siku ya kuzaliwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Irene Uwoya.

H Baba ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa muigizaji huyo kwa kusema kuwa kuachana kwao siyo sababu ya wao kutotakiana heri.

Mwanamuziki huyo kwa sasa ni mume wa mwigizaji Flora Mvungi amemtakia kheri Irene Uwoya kwa kupost picha yake Instagram na kumpa ujumbe kuwa kuachana siyo vita mpaka washindwe kutakiana kheri katika maisha yao ya kila siku.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram H Baba ameandika “Kuachana siyo vita ya mimi nisikutakie mafanikio mema kwenye maisha yako ukweli unaujua wewe na mimi. Kikubwa tunaheshimiana, uliolewa nikaoa, una mtoto nina watoto, Una Ndiku mimi nina Mvungi wangu. Mapenzi siyo vita uwoya kazaliwa Happy Birthday Irene Uwoya ‘Allah’ akuongoze vyema kwenye maisha yako na mafanikio yako nakuombea baraka telee kwenye maisha yako”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *