Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefutiwa kesi ya kushindwa kutunza silaha baada ya mahakama kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo, na kuamuru arudishiwe mkoba wenye silaha yake.

Gwajima na wenzake watatu wamefutiwa mashtaka hayo mbele ya hakimu mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkehe.

Katika kesi hiyo ambayo Gwajima alikuwa akisimamiwa na Wakili Peter Kibatala, washtakiwa hao walikuwa wakidaiwa kuwa Machi 29, 2015 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A walikutwa wakimiliki Bastola aina ya Berretta yenye namba ya siri CAT 5802 bila ya kuwa na kibali toka kwa mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

Washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 32 (1) na cha 34 (1) (2) na(3) cha sheria ya Silaha na Milipuko sura ya 223 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Siku ya tukio washtakiwa hao pia walikutwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya Shotgun.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *