Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa anakaribia kustaafu kufundisha soka na hataitakuwa miaka 65 kama alivyodhani awali.

Muispania huyo amewahi kuifundisha klabu ya Barcelona ka mafanikio makubwa kisha Bayern Munich kabla ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini Man city.

Gurdiola mwenye umri wa miaka 45 amesema kuwa hatoweza kufundisha mpira hadi miaka 60-65 na anafikiria kuanza mchakato wa kusataafu kutokana na umri wake alionao sasa.

Kocha huyo ameshinda vikombe 14 katika miaka minne akiwa na Barcelona, ikiwa ni pamoja na vikombe vitatu vya La Liga na viwili vya ligi ya mabingwa Ulaya.

Alipumzika mwaka mzima kabla ya kujiunga na Bayern Munich na kuwaongoza kupata vikombe vitatu vya ligi kuu licha ya kukosa ligi ya mabingwa Ulaya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *