Kocha wa Manchester City, Pep Gurdiola amesema timu yake lazima iongeze kiwango kama inataka kushinda ligi kuu nchini Uingereza msimu huu.

Manchester City inaongoza ligi kwasasa baada ya kushinda mechi nne na kutimiza points 12 moja ya mechi walizoshinda ilikuwa dhidi ya Manchester United siku ya jumamosi katika uwanja wa Old Trafford.

Manchester City mwisho wa kutwaa kombe la ligi nchini Uingereza ilikwa mwaka 2014 chini ya kocha Manuel Pellegrini aliyetimuliwa mwisho wa msimu

Kwa upande mwingine Manchester City leo inatarajiwa kucheza dhidi ya Monchengladbach kwenye mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katika uwanja wa Etihad.

Gurdiola amesema kuwa mechi hiyo ni muhimu kwa upande wake na watahakikisha wanashinda mechi hiyo kwasababu wanancheza katika uwanja wa nyumbani hivyo watafanya juu chini ili waweze kuibuka na ushindi.

Naye kocha wa Monchengladbach, Andre Schubert amewaelezea wapinzani wao City kwa kusema ni timu bora kwasasa huku akisisitiza uhenda City ikatwaa ubingwa wa nyumbani pamoja na ligi ya mabingwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *