Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amewataka wachezaji wake kucheza kwa nidhamu katika hatua ya timu 16 bora kwenye ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Monaco leo.

Gurdiola ameshinda taji hilo mara mbili kama kocha na hakufeli kuifikisha timu hizo katika nusu fainali mara saba.

Manchester City walifika katika hatua ya nusu fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara ya kwanza msimu uliopita na wameendelea katika hatua ya mtoano mara nne pekee.

Gurdiola amesema kuwa watu wanaweza kufikiria Manchester City wanastahili kuwa hapa lakini klabu nyingi kubwa hazijafika hapa.

Kiungo wa kati wa City Kevin de Bruyne anarudi uwanjani akiwa amefunga magoli matano katika mechi 32 alizoshiriki msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *