Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa ni vigumu kwa kikosi chake kuwafikia Chelsea ambayo ndiyo kinara wa ligi kuu nchini Uingereza.

Manchester City imepanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi baada ya jana kushinda 3-0 dhidi ya Hull City na kufanikiwa kuwa nyuma kwa pointi 7 dhidi ya Chelsea.

Kikosi hicho cha Antonio Conte awali kiliweka rekodi ya kushinda mara 12 katika ligi ya Uingereza baada ya kuichapa Bournemouth 3-0.

Gurdiola amesema kuwa ”Liverpool ilikaribia taji hilo mwaka mmoja uliopita kwa sababu walikuwa na mechi moja kwa wiki ,na ni hivyo ndivyo ilivyokuwa na Leicester.Mara hii Chelsea na Liverpool wana fursa”.

Mwaka jana Liverpool na Chelsea zimeshindwa kufuzu katika mashindano ya Ulaya baada ya kumaliza wa nane na 10 mtawalia katika ligi ya Uingereza mwaka uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *