Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amemmwagia sifa mchezaji wake Gabriel Jesus baada ya kuisaidia Manchester City kupata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Westham United kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Jesus mwenye umri wa miaka 19 alifunga bao lake la kwanza na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa City kufunga na kutoa pasi ya bao akicheza kwa mara ya kwanza dakika zote tisini.

Guardiola amesema mchezaji huyo ameuzoea kwa haraka uchezaji wa City na ligi ya Uingereza hivyo atakuwa na muendelezo mzuri.

Michezo mingine ya jana usiku ya ligi hiyo, ilishuhudiwa Manchester United, ikipata sare ya 9, kwenye ligi ya msimu huu baada ya kutoka bila ya kufungana na Hull City, kwenye uwanja wao wa Old Trafford.

Mchezo unaokuja Manchester United ikishinda na City ikafungwa United inabaki palepale katika nafasi ya sita.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *