Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekanusha habari zilizoenea kwamba amewaambia wachezaji wake kutofanya mapenzi baada ya sita usiku.

Guardiola amesema kwamba hakuwaambia wachezaji kuhusu swala hilo la kutofanya mapenzi baada ya sita usiku jambo ambalo si la kweli kabisa.

Kocha huyo amesema kwamba “hawezekani kucheza mpira bila kufanya mapenzi na mwenza wako”

Kauli hiyo ya Gurdiola inakuja kufuatia habari alizosema kiungo wa timu hiyo Samiri Nasri ambaye kwasasa yupo Sevilla kwa mkopo baada ya kusema ya kulaumu sheria za gurdiola za kuwakataza wachezaji wake wasifanye mapenzi baada ya sita usiku..

Nasri amesema hakuruhusiwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Manchester City baada ya kipindi cha kujiandaa na msimu mpya kutokana na kuzidi uzito.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *